Kundi la kina Navy Kenzo laula Marekani

Navy Kenzo

Muktasari:

App hiyo ya simu inatarajiwa kuzinduliwa LEO katika tamasha la 'Mwendokasi Festival' litakalofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama.

Dar es Salaam. Kundi la muziki wa kizazi kipya nchini linaloundwa na Aika na Nahreel, Navy Kenzo, limeingia mkataba wa kuwa mabalozi wa Klobaa App ya nchini Marekani.

App hiyo ya simu inatarajiwa kuzinduliwa LEO katika tamasha la 'Mwendokasi Festival' litakalofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama.

App hiyo ni mara ya kwanza kuingia Afrika na inazinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.