Lyon yamtaka Chicharito

Muktasari:

Lyon inasaka mshambuliaji wa kuziba pengo la Alexandre Lacazette anayetakiwa na Atletico Madrid.

Paris, Ufaransa. Miamba ya Ufaransa, Lyon  imeweka mezani ofa ya Euro 12 milioni  mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Javier Hernandez.

Lyon inasaka mshambuliaji wa kuziba pengo la Alexandre Lacazette anayetakiwa na Atletico Madrid.

Lyon pia inafuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Chelsea, Bertrand Traore anayecheza kwa mkopo Ajax.

Traore ni moja ya wachezaji walioiongoza Ajax kucheza fainali ya Europa Ligi na kufungwa na  Man United.