Friday, April 21, 2017

Mabondia kuzichapa Arusha Mei Mosi

 

By Yohana Challe, Mwananchi

Arusha: Mabondi 14 wanatarija kupanda ulingoni Mei Mosi ili kuhamashisha mchezo huo katika mikoa ya Arusha na Manyara.

Pambano hilo limeandaliwa na chama cha ngumi mkoa wa Arusha (AABA) katika kuhamasisha mchezo huo wa vijana.

Mwenyekiti wa AABA, Salimu Bilali alisema pambano hilo litafanyika wiki ijayo na majina ya mabondia watakaopanda ulingoni yatawekwa hadharani.

"Kwa kuanza tumeanza kwa kushirikiana na majirani zetu Manyara katika kuandaa mapambano hayo, hapo baadaye tutashirikiana na wenzetu wa Dar es Salaam, Ruvuma, Mbeya na hata Mwanza,” alisema Bilali.

Kocha wa ngumi mkoani hapa Mark Nyitika alisema kufanyika kwa mapambano hayo kutasaidia kuongeza hamasa kwa vijana wanaopenda ngumi ikiwa nadra kufanyika hapa Arusha.

-->