Madini FC yajipanga kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao

Muktasari:

Kocha Mkuu wa Timu hiyo Adallah Juma alisema kuwa pamoja kunasa wachezaji hao kutoka timu za Ligi Kuu tayari kuna wachezaji wengine saba ambao wamejiunga na timu hiyo wakitoka kwenye timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Uongozi wa Madini FC ya jijini Arusha umesema upo katika mikakati mizito ya kukijenga kikosi chake ili kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao na umefanikiwa kunasa nyota watatu waliowahi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha Mkuu wa Timu hiyo Adallah Juma alisema kuwa pamoja kunasa wachezaji hao kutoka timu za Ligi Kuu tayari kuna wachezaji wengine saba ambao wamejiunga na timu hiyo wakitoka kwenye timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

“Sitaweza kukutajia jina la mchezaji hata mmoja kwa sasa kutokana na Muda huu kila timu inasikiliza mwenzake amefanya nini ndio na wao wafanye usajili, muda ukifika nitawaweka wazi wachezaji wapya na hata watakao temwa,” alisema.