Majeruhi Kuitesa Yanga Michuano ya Sportpesa

Muktasari:

Mwambusi alisema kuwa kutokana na matatizo hayo asilimia kubwa ya wacheza wanapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hawakuweza kusafiri na wenzao walikuja Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC.

Arusha. Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya Yanga Juma Mwambusi amesema kikosi cha timu hiyo kinakabiliwa na majeruhi wengi kuelekea katika michuano ya Sportpesa yanayotarajia kuanza kutimua vumbi june 5.

Mwambusi alisema kuwa kutokana na matatizo hayo asilimia kubwa ya wacheza wanapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hawakuweza kusafiri na wenzao walikuja Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC.

“Timu ya Yanga ilikuwa inashiriki michuano mengi ukianza ile ya Ligi kuu Tanzania Bara ambayo tumefanikiwa kutetea ubingwa wetu mara tatu mfululizo, michuano ya Shirikisho (FA), klabu bingwa Afika na baada ya kutolewa tukawa tunashiriki michuano ya shirikisho Barani Afrika”

“Michuano hiyo yote wachezaji walikuwa wanafanya kazi kwa ajili ya kutetea timu, na Taifa lao ndio maana baada ya kumaliza ligi kuu wakapewa muda wa kupumizika hasa wale ambo wamecheza michezo mingi tangu kuanza kwa msimu” Alisema Mwambusi.

Licha ya Mwambusi kutoweka bayana majina ya wachezaji waliopewa mapumziko aliongeza kuwa malengo yao ni kuhakikisha wananyakua ubingwa wa michuano ya Sportspesa.