Man City yamtaka Rose

Muktasari:

  • Kocha wa City, Pep Guardiola anataka kufanya mabadiliko katika safu yake ya mabeki wa pembeni ambapo wachezaji wake wengi wamevuka miaka 30 na inadaiwa kuwa anamfungia kazi Rose ambaye ni mmoja kati ya mabeki bora wa pembeni kwa sasa.

London, England.MANCHESTER City ina uhakika wa kumnasa beki wa kushoto wa Tottenham, Danny Rose huku ikiandaa dau la Pauni 50 milioni kwa staa huyo wa England wakati huu Tottenham ikijiandaa kuziba pengo lake kwa kumchukua Luke Shaw wa Manchester United.

Kocha wa City, Pep Guardiola anataka kufanya mabadiliko katika safu yake ya mabeki wa pembeni ambapo wachezaji wake wengi wamevuka miaka 30 na inadaiwa kuwa anamfungia kazi Rose ambaye ni mmoja kati ya mabeki bora wa pembeni kwa sasa.