Monday, June 19, 2017

Man United kula mshiko wa Ronaldo kinoma kinoma

 

 Manchester United itavuna fedha ya kutosha kwenye mauzo ya Cristiano Ronaldo hata kama wao watamnyakua mshambuliaji huyo wa Real Madrid.

Achana na faida watakayovuna kwa mauzo ya jezi kama staa huyo atarudi Old Trafford, au mauzo ya tiketi watakayouza kutokana na usajili huyo, Fifa inafichua kwamba Man United itavuna asilimia 2.5 ya ada itakayolipwa kwenye usajili wa Ronaldo kama atauzwa na Real Madrid kwenda kwenye timu nyingine.

PSG na timu za China ndizo zinazopewa nafasi kubwa ya kuipiku Man United kwenye usajili wa Ronaldo.

-->