Man United kusajili wanne tu

Muktasari:

Uongozi wa klabu hiyo ulitoa taarifa kwamba watafanya kama walivyofanya miezi michache iliyopita kwa Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba.

Man United kusajili wanne tu

Klabu ya Manchester United imedokeza usajili wake utahusisha wachezaji watatu au wanne tu ambao ni maalumu kwenye nafasi ya mshambuliaji, mabeki wa kati na viungo.

Uongozi wa klabu hiyo ulitoa taarifa kwamba watafanya kama walivyofanya miezi michache iliyopita kwa Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba.

Kocha Jose Mourinho alisema suala la usajili klabuni hapo linapaswa kufanyika kwa mkakati maalumu kulingana na mahitaji halisi.

Hata hivyo BBC Sport lilieleza kwamba mipango ya Mourinho huenda imelenga zaidi kupata saini ya wachezaji kama Griezmann, Andrea Belotti, Michael Keane na Victor Lindelof.