Man United yamkamia Guardiola

Muktasari:

Manchester United iliyopo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, wataonyeshana ubabe na kikosi hicho cha Pep Guardiola katika dimba la Etihad, huku kila timu ikiwania kumaliza katika nafasi nne za juu.

London, England. Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera amesema mechi yao dhidi ya Manchester City keshokutwa Alhamisi itakuwa ya kufa mtu kutokana na kila timu kucheza kufa kupona ili ipate pointi tatu.

Manchester United iliyopo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, wataonyeshana ubabe na kikosi hicho cha Pep Guardiola katika dimba la Etihad, huku kila timu ikiwania kumaliza katika nafasi nne za juu.

Herrera (27) alizungumzia umuhimu wa mchezo huo akisema kwamba, itakuwa ni mchezo usiotabirika kutokana na kila timu kuwa na rekodi nzuri ya kushinda hivi karibuni.

Alisema, “Utakuwa mchezo wa kufunga msimu. Tupo nyuma pointi moja nyuma yao na iwapo tutashinda tutakuwa na nafasi nzuri ya kumaliza  kwenye nafasi nne za juu, lakini wakishinda itatuwia vigumu kufikia mipango yetu