Manchester City watambulisha jezi mpya Marekani

England. Manchester City imetambulisha jezi zake mpya wakati wa ziara ya mechi za kirafiki nchini Marekani.

Timu hiyo imeanza kuonyesha jezi zao mpya za rangi ya damu ya mzee ambazo waliwahi kuzivaa mwaka 1956 kwenye mashindano ya Kombe la FA.

Pia, jezi hizo mpya walitarajia kuvaa kwenye mechi yao ya kirafiki dhidi ya Real Madrid jijini Los Anges, Marekani.

Nyota wa klabu hiyo; Leroy Sane, Ederson na Danilo walichaguliwa kuvaa jezi hizo kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuzitambulisha huku Phil Foden akivaa jezi ya kijani.

Manchester City iliambulia kipigo kwenye mechi yakeya kirafiki iliyochezwa wiki iliyopita dhidi ya Manchester United, huku Kocha Pep Guardiola akibaki kimya kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na baadhi ya wachezaji wake.