Manchester United imebakiza wachezaji wawili tu usajili huu

Kocha Jose Mourinho amewaacha hoi mashabiki wa klabu hiyo baada ya kumrushia kijembe Gareth Bale kuwa hana mpango wa kumnunua kwa sababu hawajazungumzia jambo hilo.

Mourinho aliyasema hayo kuelekea mechi yao ya kirafiki dhidi ya Real Madrid huku akifafanua kwaba katika msimu huu amebakiza nafasi mbili za kiungo na mshambuliaji wa kushoto.

Kocha huyo maarufu The Special One alikisifu kikosi chake, huku akisema anaamini nafasi zilizobaki atasajili wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao kwa sasa hawezi kuwataja.