Manchester United imebakiza wachezaji wawili tu usajili huu

Muktasari:

  • Mourinho aliongeza kuwa katika msimu huu amebakiza nafasi mbili ambazo ni kiungo na mshambuliaji wa kushoto.

Kocha Jose Mourinho amewaacha hoi mashabiki wa klabu hiyo baada ya kumrushia kijembe Gareth Bale kuwa hana mpango wa kumnunua kwa sababu hawajazungumzia jambo hilo.

Mourinho aliongeza kuwa katika msimu huu amebakiza nafasi mbili ambazo ni kiungo na mshambuliaji wa kushoto.

Kocha huyo maarufu The Special One alikisifu kikosi chake, huku akisema anaamini nafasi zilizobaki atasajili wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao kwa sasa hawezi kuwataja.