Mashabiki Dodoma wafurika kuwapokea mabingwa Area C

Muktasari:

  • Ilikuwa ni nderemo na vifijo katikati ya mji wa Dodoma na kuzungukia pande zote za mji huo msafara wa timu hiyo ulipokuwa ukipita.

 Nderemo na shangwe zilitawala jana Jumamosi mjini Dodoma wakati timu ya Area C iliporejea kutoka mkoani Tabora ilipokuwa imekwenda kuwakilisha mkoa kwenye Ligi ya Mabingwa wa mikoa na kufanikiwa kuwa bingwa wa kituo hicho.

Ilikuwa ni nderemo na vifijo katikati ya mji wa Dodoma na kuzungukia pande zote za mji huo msafara wa timu hiyo ulipokuwa ukipita.

Timu hiyo imefanikiwa kupanda daraja ambapo watacheza daraja la pili msimu ujao.

Area C imefanikiwa kuwa bingwa wa Kituo C cha Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kilichokuwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa kumaliza mechi zake 6 na kukusanya pointi 14.