Mayanga mfumo uleule

Muktasari:

Mayanga ambaye ni kocha wa muda wa Taifa Stars, alisema kuwa mfumo wa 4-4-2 katika mchezo uliopita na ndio atautumia dhidi ya Burundi huku akiwa na imani kuwa vijana hao wa Pierre Nkurunzinza wajiandae na kipigo.

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema katika mchezo wa kirafiki wa kesho dhidi ya Burundi atatumia mfumo ule ule aliotumia kuwaua Botswana wikiendi iliyopita.

Mayanga ambaye ni kocha wa muda wa Taifa Stars, alisema kuwa mfumo wa 4-4-2 katika mchezo uliopita na ndio atautumia dhidi ya Burundi huku akiwa na imani kuwa vijana hao wa Pierre Nkurunzinza wajiandae na kipigo.

"Kwa wachezaji ambao nipo nao katika timu wanaweza kufiti vizuri katika mfumo wa 4-4-2, ndio ambao nilianza kuutumia katika mchezo dhidi ya Botswana na tulipata matokeo chanya," alisema.

"Lakini kama wapinzani wataweza kugundua na kutuzuia tunaweza kubadilisha na kutumia mfumo wa 4-5-1, ambao naweza kupunguza winga mmoja na kuongeza kiungo mshambuliaji ili kusaidiana na viungo wa kati na kufanya mechi kuwa rahisi kwa upande wetu," alisema Mayanga.