Monday, June 19, 2017

Mayay ajitosa kuwania urais wa TFF katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12, Dodoma

 

By Charles Abel,Mwananchi cabel@mwananchi.co.tz

Nahodha wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay amechukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),  utakaofanyika Agosti 12.

Mayay amechukua fomu hizo saa 5 asubuhi akiwa sambamba na mchezaji wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhan anayewania umakamu wa Rais.

Watia nia hao walisindikizwa na umati wa wanasoka wa zamani ambao wengi walibeba ujumbe wa kuwaunga mkono Mayay na Ramadhan.

Wachezaji wa zamani wamejikusanya kwenye shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kumsindikiza Mayay kwenda kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais wa TFF.

Baadhi ya wachezaji hao ni Thomas Kipese, Madaraka Selemani, Jamhuri Kihwelu, Mohammed Hussein 'Mmachinga ', Bakari Malima 'Jembe Ulaya ' na  Salum Swedi 'Kussi'.

-->