Medeama wawachosha Yanga

Muktasari:

  • Awali, viongozi wa Medeama waliowapokea Yanga mjini Accra, waliwatoa wasiwasi wachezaji na viongozi hao kuhusu umbali huo wa saa tatu hadi nne, tofauti na muda halisi waliotumia njiani.

Accra, Ghana. Wachezaji wa Yanga waliduwaa kuona umbali uliopo kati ya Jiji la Accra kwenda Tarkwei ilipo klabu ya Medeama, watakayocheza nayo mechi ya Kombe la Shirikisho Afika, kesho.

Awali, viongozi wa Medeama waliowapokea Yanga mjini Accra, waliwatoa wasiwasi wachezaji na viongozi hao kuhusu umbali huo wa saa tatu hadi nne, tofauti na muda halisi waliotumia njiani.

Basi walilotumia Yanga kutoka Accra ilitumia saa tano na nusu hadi kufika katika Hoteli ya Planters, waliyopangiwa na wenyeji wao. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ pamoja na wenzake hakusita kuonyesha mshangao kuhusu taarifa za awali walizoambiwa na wenyeji wao juu ya muda watakaotumia.

Beki Juma Abdul alisema umbali huo umemshangaza kutokana na jinsi walivyokuwa wakiambiwa wakiwa Accra kabla ya kuanza safari ya kwenda Tarkwei.