Mjumbe Kamati ya Utendaji Simba apenya mchujo wagombea uchaguzi TFF

Muktasari:

  • Suru ni miongoni mwa majina sita yaliyopenya kwenye mchujo wa kuwania kuiwakilisha mikoa hiyo katika kamati ya utendaji ya TFF kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mjini Dodoma, Agosti 12 huku wengine wakiwa ni Hussein Mwamba, Mohamed Aden, Musa Sima,Stewart Masima na George Benedict.

Kitendo cha kupenya kwenye mchujo wa awali kwenye mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kimemshusha presha mgombea ujumbe wa kuwakilisha mikoa ya Singida na Dodoma, Ally Suru ambaye ameishukuru kamati ya uchaguzi kwa kupitisha jina lake.

Suru ni miongoni mwa majina sita yaliyopenya kwenye mchujo wa kuwania kuiwakilisha mikoa hiyo katika kamati ya utendaji ya TFF kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mjini Dodoma, Agosti 12 huku wengine wakiwa ni Hussein Mwamba, Mohamed Aden, Musa Sima,Stewart Masima na George Benedict.

Mgombea huyo ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, aliliambia gazeti hili kuwa kitendo cha kamati kupitisha jina lake ni ishara njema kuelekea uchaguzi huo ambao unasubiriwa kwa hamu na wadau wa soka nchini.