Mkwassa aita 24 kuivaa Ethiopia

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.
Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.
Nyota wa Stars walioitwa  ni:
Makipa: Deogratius Munishi (Yanga), Said Kipao (JKT Ruvu) na Aishi Manula (Azam)
Mabeki: Shomari Kapombe, David Mwantika ( Azam), Juma Abdul, Vincent Andrew, Mwinyi Haji (wote Yanga) Mohamed Hussein (Simba) na James Josephat (Prisons)
Viungo:  Himid Mao (Azam), Mohammed Ibrahim, Jonas Mkude,  Muzamiru Yassin, Jamal Mnyate na Shiza Kichuya (wote  Simba), Simon Msuva,Juma Mahadhi (Yanga), Hassan  Kabunda (Mwadui ).
Washambuliaji: Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Mbwana Samatta(Genk) Elius Maguli ( Fanja), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).