Monaco yamweka sokoni Mbappe

Muktasari:

  • Mbappe, 18, ameliteka soka la Ulaya kwa sasa baada ya kutesa katika Ligi Kuu ya Ufaransa huku akiifikisha Monaco katika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kuitoa Manchester City katika pambano la mtoano.

Monaco, Ufaransa.MONACO imepanga bei ya staa wake kinda, Kylian Mbappe kuwa Pauni 130 milioni kwa klabu yoyote inayomtaka huku ikidaiwa kuwa Manchester United inaongoza katika mbio za kumtaka Mfaransa huyo.
Mbappe, 18, ameliteka soka la Ulaya kwa sasa baada ya kutesa katika Ligi Kuu ya Ufaransa huku akiifikisha Monaco katika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kuitoa Manchester City katika pambano la mtoano.