Mourihno amnasa nyota wa Inter Milan

Muktasari:

Gazeti la SunSport liliripoti Machi kuwa Jose Mourinho alisafiri kwenda Zagreb kufanikisha suala la usajili huyo.

Mourihno amnasa nyota wa Inter Milan

London, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho yuko mbioni kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan, Ivan Perisic kwa gharama ya pauno 40milioni.

Mshambuliaji Perisic (28), amekubali kupokea mshahara wa pauni100,000 kwa wiki na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajili Old Trafford msimu huu.

Gazeti la SunSport liliripoti Machi kuwa Jose Mourinho alisafiri kwenda Zagreb kufanikisha suala la usajili huyo.

Bosi huyo wa Man United yupo tayari kuanza usajili baada ya kufanikiwa kupata ubingwa wa Europa Ligi na kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Chelsea na Paris Saint-Germain nazo zilikuwa zinamtaka Perisic na miamba ya Ufaransa ipo tayari kutoa fedha pamoja na winga Angel Di Maria kufanikisha usajili huo.