Mourinho alia na ratiba

Kocha Jose Mourinho

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Man United amesisitiza hatodharau mashindano hayo kwa kupanga kikosi dhaifu, kama Manchester City walivyofanya wakati walipotolewa na katika Kombe la FA na Chelsea mwaka jana.
  • Man United imefuzu kwa hatua ya 16 bora ya Europa Ligi kwa kuifunga St-Etienne kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-0 juzi na leo atajua mpinzani wake katika ratiba itakayopangwa jijini Nyon.

London, England.Kocha Jose Mourinho amelalamikia ratiba ya robo fainali ya Kombe la FA ya Manchester United kucheza na Chelsea Jumatatu usiku mwezi ujao ikiwa ni siku tatu kabla ya mchezo wao wa Europa Ligi.

Kocha huyo wa Man United amesisitiza hatodharau mashindano hayo kwa kupanga kikosi dhaifu, kama Manchester City walivyofanya wakati walipotolewa na katika Kombe la FA na Chelsea mwaka jana.

Man United imefuzu kwa hatua ya 16 bora ya Europa Ligi kwa kuifunga St-Etienne kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-0 juzi na leo atajua mpinzani wake katika ratiba itakayopangwa jijini Nyon.

Kikosi cha Mourinho kitacheza mechi ya marudiano ya Europa Ligi ugenini saa 72 baada ya kucheza na Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumatatu, Machi 13.

Mourinho ameilaumu FA na viongozi wa televisheni kwa kuhamishja mechi hiyo muda mfupi kabla ya Man United kucheza mchezo wake wa juzi usiku na amewashutumu kwa kushindwa kujali kuhusu klabu yake.

Amehaidi kutochezesha timu dhaifu, kama walivyofanya City mwaka jana na kufungwa mabao 5-1 na Chelsea katika Kombe la FA kabla ya mechi yao ya ugenini dhidi ya Dynamo Kiev.

Mourinho alisema: 'Nimeshangazwa kweli kwa uamuzi huu kufanywa kabla ya ratiba ya Ulaya kwa sababu sasa hakuna anayejua tutacheza na nani na wapi, tutaanzia nyumbani au ugenini.

'Nafikiri tunacheza na Chelsea siku ya Jumatatu na mechi yako ya Ulaya umepangwa kucheza Russia, Uturuki au Ugiriki? Nafikiri tena nafasi ya klabu na soka la England kama hakuna mtu anayejari lolote kuhusu hilo.

Man United imepata pigo kwa viungo wake Henrikh Mkhitaryan na Michael Carrick wote kuumia katika ushindi wao wa bao1-0 dhidi ya St-Etienne hivyo hawataweza kucheza mechi ya Jumapili katika fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa Wembley.

Mourinho ametadhalisha kuwa Man United itapata majeruhi wengi kutokana na ratiba iliyopo mbele yake.