Mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich aamua kustaafu soka

Muktasari:

  • Mkongwe huyo aliyekuwa akicheza nafasi ya ushambuliaji, amecheza jumla ya mechi 100 ikiwamo za kwenye taifa lake.

Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich na mchezaji wa kimataifa wa Croatia, Ivica Olic ametangaza kustaafu soka.

Mkongwe huyo aliyekuwa akicheza nafasi ya ushambuliaji, amecheza jumla ya mechi 100 ikiwamo za kwenye taifa lake.

Pia, alifanikiwa kuifungia mabao Crotia kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kati ya mwaka 2002 mpaka 2014. Olic ameamua kutundika daruga akiwa amefikisha miaka 37.

Mchezaji huyo alianza kusakata soka nchini Crotia kwenye klabu ya Marsonia kabla ya kujiunga na Ligi Kuu ya Urusi na kunyakua mataji ya ubingwa ya ligi hiyo pamoja na taji la UEFA mwaka 2005 akiwa na CSKA Moscow.

Maisha yake ya soka ameitumikia Bundersliga kwa muda mrefu na alihamia Bayern Munich akitokea Hamburg.