Mshindi wa drafti Moro kuchomoka na mbuzi

Muktasari:

  • Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa Mjini hapo, Rashidi Matessa alisema kuwa mashindano hayo yana lenga kukusanya vijana na kukaa pamoja ili kujadili fursa mbalimbali ndani ya Manispaa ya Morogoro.

 Mashindano ya mchezo wa drafti ya Matessa Cup 2017 Manispaa ya Morogoro yamezinduliwa huku Ally Dogo akinyakua zawadi ya Sh10,000 katika mchezo wa kwanza wa mashindano hayo yanayofanyika kwenye klabu ya drafti Mawenzi mjini hapa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa Mjini hapo, Rashidi Matessa alisema kuwa mashindano hayo yana lenga kukusanya vijana na kukaa pamoja ili kujadili fursa mbalimbali ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Mratibu wa mashindano hayo, Athman Mswagala alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha wachezaji 42 na mshindi wa kwanza atapata zawadi ya mbuzi.