Mtaka ‘alia’ na kigezo cha elimu

Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT), Anthony Mtaka.

Muktasari:

  • Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili katika makao makuu ya Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), Tabata Relini,  Mtaka alisema kitendo cha katiba za vyama vya michezo kupitisha mgombea kwa kigezo cha kujua kusoma na kuandika kimechangia kuongeza idadi ya wababaishaji katika tasnia hiyo.

Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT), Anthony Mtaka amesema viongozi wengi wa vyama vya michezo ni wababaishaji ari inayochangia tasnia ya michezo nchini kutofanikiwa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili katika makao makuu ya Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), Tabata Relini,  Mtaka alisema kitendo cha katiba za vyama vya michezo kupitisha mgombea kwa kigezo cha kujua kusoma na kuandika kimechangia kuongeza idadi ya wababaishaji katika tasnia hiyo.

“Ukiangalia muundo wa vyama vyetu vingi vya michezo, watu wanaoingia kugombea na kuongoza wengi ni wababaishaji, hii kwa kiasi kikubwa inachangia kurudisha nyuma maendeleo katika tasnia hii.