Mwanjali aipa auheni Simba

Muktasari:

Beki huyo aliyeumia tangu Simba ilipocheza na Azam FC , Januari 28 ni sehemu ya nyota 28 wa timu hiyo inayojiandaa kucheza mechi hiyo ya fainali kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Dodoma. Beki wa Simba, Mzimbabwe Method Mwanjali  ameongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo baada ya kurejea mazoezi na huenda akacheza dhidi Mbao FC kesho.

Beki huyo aliyeumia tangu Simba ilipocheza na Azam FC , Januari 28 ni sehemu ya nyota 28 wa timu hiyo inayojiandaa kucheza mechi hiyo ya fainali kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

"Mwanjali amefanya mazoezi ya kumuweka fiti kwa siku tatu na yuko tayari kucheza kama kocha ataona anafaa, " alisema mratibu wa Simba, Abbas Ally

Mshindi wa mechi hiyo ya fainali atapata nafasi ya kushirki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.