Mwanjali arejea kikosini Simba

Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjali ameanza mazoezi pamoja wenzake leo asubuhi.

Muktasari:

  • Mwanjali aliumia goti lake la mguu wa kushoto wakati wa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
  • Katika mazoezi hayo, Mzimbabwe huyo alikuwa amefunga kitambaa cha kuondoa maumivu kwenye goti hilo na kufanya mazoezi ya kukimbia, kupigiana mpira na mazoezi mengine yaliyokuwa chini ya uangalizi wa daktari.

Unguja. Beki wa kati wa Simba, Method Mwanjali ameanza mazoezi pamoja wenzake leo asubuhi.
Mwanjali aliumia goti lake la mguu wa kushoto wakati wa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.
Katika mazoezi hayo, Mzimbabwe huyo alikuwa amefunga kitambaa cha kuondoa maumivu kwenye goti hilo na kufanya mazoezi ya kukimbia, kupigiana mpira na mazoezi mengine yaliyokuwa chini ya uangalizi wa daktari.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe anasema Mwanjali anaendelea vizuri.
"Kama unavyomwona, Mwanjali anaendelea vizuri na imani yangu mpaka siku ya mchezo wetu na Yanga atakuwa ameimarika kabisa."
Mwanjali anasema "namshukuru Mungu naendelea vizuri kikubwa namwomba nipone kabisa,"alisema Mwanjali.
Naye, rais Simba, Evance Aveva amefurahia kurudi kwa Mwanjali uwanjani.
"Mwanjali alikuwa ananipa wasiwasi mkubwa, lakini kwa maendeleo haya, mambo yatakuwa mazuri tu," anasema Aveva.
Simba iipo kambini Zanzibar na wachezaji wao wote ni wazima isipokuwa, Jamal Mnyate ambaye ni majeruhi.