Friday, July 21, 2017

Mzamiru afichua siri zake

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Kiungo wa Simba, Mzamiru Yasini amesema amejifunza mbinu za kiufundi akiwa na Taifa Stars, zitakazomsaidia kufanya vitu tofauti msimu ujao.

"Kupitia Stars, tumecheza na timu tofauti zenye ushindani wa juu, hilo limekuwa faida kwangu, kujiweka sawa kwa ajili ya ligi ukichukulia kwamba nitakuwa na muda mfupi wa maandalizi ya msimu unaokuja,unaoonekana kuwa na ushindani mkali," anasema.

Mbali na Stars, kumsaidia kuwa fiti, pia imemtangaza nje ya mipaka ya Tanzania kwa madai uwezo wake umeonekana dhidi ya timu walizokuwa wanacheza nazo.

"Ndoto zangu nikufika mbali, hilo linanifanya kuwa mshindani kuanzia kwenye timu yangu ya Simba, iliyofanya kocha wa Stars, Salum Mayanga, kuniona," alisema Mzamiru.

-->