Nape aipa tano TFF

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amelipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kubuni wazo la kuwa na Mfuko wa Maendeleo ya Soka (TFDF).

Muktasari:

  • Akizungumza leo (Alhamisi) kwenye hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Nape amesema mfuko huo utarahisisha upatikanaji wa rasilimali fedha zitakaosaidia kukuza soka la vijana nchini.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amelipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kubuni wazo la kuwa na Mfuko wa Maendeleo ya Soka (TFDF).

Akizungumza leo (Alhamisi) kwenye hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Nape amesema mfuko huo utarahisisha upatikanaji wa rasilimali fedha zitakaosaidia kukuza soka la vijana nchini.

"Serikali  ilikuwa inatafuta namna ya kushirikiana na kusapoti michezo lakini kwa TFF kuanza na jambo, hili tunawaunga mkono,"amesema Nape.

Pia, Nape amesema Serikali inaunga mkono maandalizi ya Serengeti Boys kabla ya kwenda Gabon kushiriki fainali za Afrika kwa vijana.