Wednesday, January 11, 2017

Nape amteua Yusuf Omari mkurugenzi wa michezo

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo,

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari. Picha na Blogu ya Jiachie 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemteua Yusuph Omari kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kujaza nafasi iliyo achwa wazi na Leornad Thadeo aliyehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Kabla ya uteuzi huo, Omari alikuwa mkufunzi mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Ardhi katika masuala ya michezo.

Nnauye  pia limshukuru aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wote, Alex Nkenyenge ambaye alifanya kazi zake kwa uadilifu na kujituma kwa kusimamia majukumu yote ya idara kwa ukamilifu.

Aidha,  ametoa wito kwa wanamichezo na wananchi  kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Omari atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.

-->