Neymar aichungulia Manchester United ikilala bao 1-0

Muktasari:

  • Wakati hali ikiwa hivyo, Kocha Jose Mourinho alipata muda wa kuzungumza na Neymar huku akisema yalikuwa ya kawaida na yasitafsiriwe tofauti.
  • Kocha huyo amekuwa akimtaja Neymar kuwa ni kati ya wachezaji aliokuwa akiwataka kutua Old Trafford, huku ikielezwa klabu ya PSG ya Ufaransa inajipanga kutoa dau nono kwa mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka mitano.

LOS ANGELES, Marekani.Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar imeifungia bao timu yake dhidi ya Manchester United katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana Jumatano  na kumalizika kwa ushindi wa bao 1-0.

Wakati hali ikiwa hivyo, Kocha Jose Mourinho alipata muda wa kuzungumza na Neymar huku akisema yalikuwa ya kawaida na yasitafsiriwe tofauti.

Kocha huyo amekuwa akimtaja Neymar kuwa ni kati ya wachezaji aliokuwa akiwataka kutua Old Trafford, huku ikielezwa klabu ya PSG ya Ufaransa inajipanga kutoa dau nono kwa mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka mitano.

Kabla ya mchezo huo uliofanyika Maryland, Neymar alikutana na Mourinho kisha kukumbatiana.

Mourinho aliwataka mashabiki kutoweka fikra zozote na kwamba hafahamu chochote kuhusu mchezaji huyo iwapo anakuja Old Trafford.