Neymar akerwa kufananishwa na Messi, Ronaldo

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Neymar

Muktasari:

  • Mchezaji huyo amesema kwamba anajiandaa kuwa nahodha wa Brazil, hivyo haoni kwamba ni sahihi wachambuzi na wachezaji wenzake kuamlinganisha na mastaa hao.

Brazil. Kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Neymar amesema anachukizwa tabia ya kumlinganisha na Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo kwenye viwango vya soka.

Mchezaji huyo amesema kwamba anajiandaa kuwa nahodha wa Brazil, hivyo haoni kwamba ni sahihi wachambuzi na wachezaji wenzake kuamlinganisha na mastaa hao.

Nyota wa Barcelona, Messi na mwenzake wa Real Madrid, Ronaldo wamekuwa wakitawala soka la dunia baada ya kushinda mara kadhaa Tuzo za Ballon d’Or kwa zaidi ya mara tisa kwa pamoja, huku wakimuacha Neymar.