Neymar hachomoki dau la Man United

Muktasari:

Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akionyesha waziwazi mapenzi yake kwa timu yake ya sasa ya Barcelona, jambo ambalo limewafanya Manchester United kuingia mfukoni na kutangaza dau kubwa ambalo litamshawishi Neymar.

London, England. Manchester United imepania kuhakikisha inamsajili nyota wa Barcelona, Neymar Jr kipindi cha kiangazi baada ya kuanzisha mazungumzo ya awali.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akionyesha waziwazi mapenzi yake kwa timu yake ya sasa ya Barcelona, jambo ambalo limewafanya Manchester United kuingia mfukoni na kutangaza dau kubwa ambalo litamshawishi Neymar.

Licha ya kwamba Mashetani hao wekundu wa London wametangaza kufanya kufuru ya usajili wa dunia kwa kulipa fedha ya uhamisho wa Pauni 170 ili kuipata huduma yake, lakini mchezaji huyo bado amekuwa akisisitiza kwamba anafurahia maisha akiwa na miamba hiyo ya Hispania.

Hilo limetokana na Neymar kufurahia muunganiko wa Lionel Messi na Luis Suarez wanapokutana wachezaji hao watatu na kuunda kikosi hatari maarufu MSN ambacho kimekuwa tishio kwa mabao.