Monday, June 19, 2017

Pele mwenyewe anamkubali Ronaldo

 

Sao Paolo, Brazil. Gwiji wa Brazil, Pele amesema kwamba hakuna ubishi kwamba kwa sasa Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.

Staa huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 32 anapewa nafasi kubwa ya kutetea tuzo yake ya Ballon d'Or baada ya kuisaidia Real Madrid kutetea ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo ametwaa  pia taji la La Liga jambo linalompa nafasi kubwa mchezaji huyo aliyetishia kuihama Real Madrid kuwa nafasi kubwa ya kubeba tuzo hiyo ya ubora wa dunia.

-->