Philippe Coutinho avutiwa dau la usajili Barcelona

London, England. Nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho anakaribia kuondoka Liverpool baada ya kukubaliana na masharti ya mkataba wa Barcelona.

Vyanzo vya habari kutoka Hispania vilidokeza kuwa raia huyo wa Brazil amekuwa akihusishwa kusajiliwa kwa dau la Pauni 89 milioni na Barcelona.

Wiki iliyopita, Kocha Jurgen Klopp alikataa ofa ya Pauni 72 milioni, huku akisisitiza kuwa atahakikisha mchezaji huyo anaendelea kubaki kwenye dimba la Anfield.