Pluijm ni zaidi ya Yanga

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm.

Muktasari:

  • Tofauti na Tanzania ambako nyota wengi wa Yanga wanajulikana kama si wote, hapa Ghana, gumzo ni Pluijm.

Accra, Ghana. Kocha wa Yanga, Hans Pluijm ndiye mtu pekee kwenye kikosi cha Yanga anayejulikana hapa Ghana.

Tofauti na Tanzania ambako nyota wengi wa Yanga wanajulikana kama si wote, hapa Ghana, gumzo ni Pluijm.

Pluijm, aliyewahi kufundisha soka nchini hapa alionekana mwenyeji na maarufu zaidi ya kikosi chake, Yanga alipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka jijini Accra juzi.

Akionekana kujuana zaidi na askari wa Uhamiaji, Pluijm aliwavuka watu wote kwenye msururu wakisubiri kukaguliwa kuingia nchini humo.