Polisi Dodoma yamtema kocha

Muktasari:

Taarifa za kutemwa kwa kocha huyo anayekidhi vigezo vya kufundisha Ligi Daraja la Kwanza kutokana na kuwa na leseni B inayotakiwa imewashangaza wadau wa soka Dodoma na kuhoji sababu za kutemwa kwake baada ya mechi moja pekee.

Dodoma. Baada ya kuiongoza timu ya Polisi Dodoma wakati ikibanwa mbavu nyumbani dhidi ya Panone kutoka Kilimanjaro, kocha James Makunja amepewa mkono wa kwa heri kwa sababu zisizojulikana.

Taarifa za kutemwa kwa kocha huyo anayekidhi vigezo vya kufundisha Ligi Daraja la Kwanza kutokana na kuwa na leseni B inayotakiwa imewashangaza wadau wa soka Dodoma na kuhoji sababu za kutemwa kwake baada ya mechi moja pekee.

Katibu mkuu wa Polisi, Michael Mtebene aliyethibitisha kutemwa kwa kocha huyo  alieleza kwamba uamuzi huo umefanyika mapema ili kutoa nafasi ya kupata kocha mpya wakati ligi ikiwa mwanzoni.