Polisi Moro yalia ukata

Muktasari:

Ofisa habari wa klabu hiyo, Clement Bazo amesema kwa sasa klabu imekumbwa na ukata wa kifedha hali inayowapa wasiwasi kuihudumia kikamilifu ligi.

Morogoro. Licha ya Polisi Morogoro kufanya vizuri katika Ligi Daraja la Kwanza, uongozi wa klabu hiyo umetangaza kukumbwa na ukata mkali kifedha na kulazimika kusaka wafadhili ili kujinurusu kiuchumi.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Clement Bazo amesema kwa sasa klabu imekumbwa na ukata wa kifedha hali inayowapa wasiwasi kuihudumia kikamilifu ligi.

Bazo amesema kuwa ina tatizo la kifedha hali inayopelekea viongozi kukuna vichwa usiku na mchana kusaka wafadhili wa kuisaidia fedha ili iendelee na malengo yake ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

“Hii timu ni moja ya timu hatari katika Ligi Daraja la Kwanza, kwanza wachezaji wana uwezo wa kuifunga timu pinzani popote pale iwe uwanja wetu wa nyumbani au ugenini na unaweza kuona tuna pointi 12 katika michezo mitano,”amesema Bazo.