Prisons kusaka washambuliaji

Wachezaji wa timu ya Tanzania Prison

Muktasari:

Kauli hiyo inakuja baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu huku mechi ya juzi  kati ya maafande hao na Mbao FC iliyochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya ikishindwa kutumia vyema nafasi nyingi za wazi walizopata ikionyesha upungufu mkubwa kwenye ushambuliaji.

Mbeya.  Benchi la Ufundi la klabu ya Tanzania Prisons limesema  kuna tatizo kubwa kwenye safu yao ya ushambuliaji na katika usajili wa dirisha dogo wanatarajia kufanya mabadiliko ya maana zaidi kwenye safu hiyo.

Kauli hiyo inakuja baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu huku mechi ya juzi  kati ya maafande hao na Mbao FC iliyochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya ikishindwa kutumia vyema nafasi nyingi za wazi walizopata ikionyesha upungufu mkubwa kwenye ushambuliaji.

Katika mechi ya juzi, Prisons, ilionekana kutawala mchezo huo vipindi vyote viwili na kupata kona zaidi ya 15, huku ikikosa umakini wa umaliziaji licha ya kupata nafasi nzuri za kufunga  mabao mengi.

Mbali na kupata kona hizo, wachezaji Salum Bosco, Benjamin Asukile, Salum Kimenya na Kazungu Mashauri kila mmoja alikosa nafasi za wazi kwa kupiga mipira ya kichwa, lakini yote waliipaisha juu ya lango la Mbao.