Prisons waipania Mbao leo

Wachezaji wa timu ya Tanzania Prison.

Muktasari:

  • Prisons ambayo katika mechi za hivi karibuni imekuwa na matokeo mabaya, Jumatano wiki hii waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani Sokoine, Mbeya kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Stand United na wachezaji walionekana  kucheza mpira safi muda wote.

Mbeya. Baada ya Tanzania Prisons kuwabamiza wababe wa Yanga na Azam, Stand United bao 2-1,  imejigamba kwa kusema wanasubiri kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza leo.

Prisons ambayo katika mechi za hivi karibuni imekuwa na matokeo mabaya, Jumatano wiki hii waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani Sokoine, Mbeya kwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Stand United na wachezaji walionekana  kucheza mpira safi muda wote.

Kocha msaidizi wa maafande hao, Shaaban Kazumba alisema kikosi chake kilikuwa na tatizo moja kwenye safu ya ushambuliaji kutoelewa wakiwa uwanjani lakini Kocha Mkuu, Meja Mstaafu, Abdul Mingange amejitahidi kuwaweka sawa na sasa wameonekana kufanya vizuri hivyo mechi ya kesho hawatakuwa na muda wa kupoteza.