Monday, June 19, 2017

Prisons yasaka mshambuliaji mpya wa kuongezea changamoto Hangaya, Jeremiah

 

By Thomas Ng’itu

Kocha wa Tanzania Prison, Abdallah Mohammed 'Baresi' ameamua kuingia darasani kusaka leseni daraja A la ukocha.

Pamoja na kuwa masomoni bado anaendelea na usajili wa wachezaji anaowataka kwa misimu ujao.

Prison iliporomoka katika msimu uliopita hasa katika nafasi ya ushambuliaji baada ya washambuliaji wake Victor Hangaya na Jeremiah Juma kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Baresi alisema katika ripoti yake amependekeza apatikane mshambuliaji mzuri anayeweza kuongeza nguvu kwa waliopo na kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri msimu ujao.

Alisema kulikuwa na mabadiliko ya benchi la ufundi, lakini hayakuwa mabadiliko makubwa sana ambayo yangemfikia yeye.

-->