Rashford, Rooney kuongoza mauaji ya Man City

Muktasari:

  • Bosi huyo wa Man United amepanga kumwanzisha Rashford kutoka na mazoezi yake ya mwisho ya mechi hiyo. Huku nahodha Rooney aliyerejea Jumapili iliyopita na kufunga dhidi ya Burnley ataanza katika kikosi hicho ambacho kitamkosa Paul Pogba.

London, England .Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amepanga kuwaanzisha pamoja na Marcus Rashford na Wayne Rooney dhidi ya Manchester City leo saa 4:00 usiku.

Bosi huyo wa Man United amepanga kumwanzisha Rashford kutoka na mazoezi yake ya mwisho ya mechi hiyo. Huku nahodha Rooney aliyerejea Jumapili iliyopita na kufunga dhidi ya Burnley ataanza katika kikosi hicho ambacho kitamkosa Paul Pogba.

Mourinho aliwasifu wachezaji wake wa kwa kucheza kwa kujituma, huku akitegemea kurejea kwa mabeki wake Phil Jones na Chris Smalling.

Kuelekea katika mchezo huo wa usiku kwenye Uwanja wa Etihad, kocha huyo wa Man United anajua mapungufu ya safu yake ya ulinzi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya majeruhi.