Real Madrid sasa kumsajili Mbappe juu kwa juu

Hispania. Klabu ya Real Madrid imeibua upya suala la usajili wa  mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe baada ya kusema imekubali kumnunua mchezaji huyo kwa dau la Pauni 161 milioni, lakini itamuacha kwa mkopo klabuni kwake kwa msimu mmoja zaidi.

Suala la Mbappe limeibuka leo Jumanne baada ya kimya cha muda mrefu kutokana na uongozi wa klabu hiyo kuzima purukushani za kumsajili mchezaji huyo walipotangaza kuwa hawana mpango wa kumuuza.

Real Madrid imeamua kumrudia Mbappe baada ya kumuuuza mchezaji wake Alvaro Morata. Sasa suala la Mbappe imelivalia njuga.

Vyanzo vya habari vimedokeza kuwa mchezaji huyo atakuwa akipokea mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki.