Rocky City Marathon kutikisa Mwanza leo

Muktasari:

  • Mbio hizo zinazofanyika kwa mara  ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na Kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na Mkoa wa Mwanza.

Mwanza. Mashindano ya Rock City Marathon yanafanyika leo jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza huku wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu wakitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

Mbio hizo zinazofanyika kwa mara  ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na Kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na Mkoa wa Mwanza.

Lengo la mbio hizo imeelezwa kuwa ni kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio vilivyoko kanda ya Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.

Msemaji wa waandaaji wa mbio hizo, Mathew Kasonta aMEsema maandalizi yote yamekamilika, ikiwamo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.