Monday, July 17, 2017

Ruvu Shooting yaibomoa Toto Africans

 

By THOBIAS SEBASTIAN

Dar es Salaam. Ruvu Shooting ilikamilisha usajili wa winga Jamali Sudy kutoka Toto Africans ya Mwanza.

Ofisa habari wa timu hiyo mwenye maneno mengi Masau Bwire alisema wamemsajili winga huyo kutokena na mapendekezo ya kocha wa Malale Hamsini.

Masau alisema licha ya kukamilisha usajili wa winga huyo uongozi wa Ruvu Shooting upo Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji kadhaa kutoka visiwani humu ambao majina yao hawatayatangaza sasa.

“Baada ya kumaliza usajili wa Sudy, uongozi wetu umeweka kambi visiwani Zanziba kukamilisha usajili wa wachezaji kadhaa ambao tumeshakubaliana nao kila kitu kilichobaki ni kuwatimizia yale mahitaji ambayo walikuwa wanahitaji ili kusaini mkataba,” alisema.

“Jambo ambalo linafanya tusiyatangaze majina ya wachezaji hao kutoka Zanzibar ni kwamba kati yao kuna wengine wanamikataba na timu zao kwahiyo tunataka kumaliza kwanza kila kitu na baada ya hapo tutatangaza,” alisema Masau.

-->