Serengeti Boys kujipima Guinea, Rwanda

Muktasari:

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema  mechi hizo ni nje ya michezo ya mitatu ya kirafiki itakayopigwa wakati  timu itakapoweka kambi nje.


Dar es Salaam. Timu ya Vijana Serengeti Boys itacheza michezo minne ya kujipima nguvu kabla ya kwenda nje ya nchi kuweka kambi ya mwezi mmoja katika michezo itapigwa kati ya Machi 13 hadi Aprili 12 .

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema  mechi hizo ni nje ya michezo ya mitatu ya kirafiki itakayopigwa wakati  timu itakapoweka kambi nje.

"Hii ni program ya kocha na tayari tumeomba kwa wenzetu Guinea, Kenya, Rwanda na Burundi. Tunakusudia mechi hizo zitachezwa Dar es Salaam au kwenye miji mingine mikoani,"amesema Lucas

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Soka la Vijana cha TFF, Kim Poulsen amesema kucheza mechi nyingi za kujipima nguvu kutaisaidia Serengeti Boys kutimiza lengo la kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Wakati huohuo, TFF imesema wiki ijayo itatangaza utaratibu wa Watanzania kuichangia Serengeti Boys.