Serengeti Boys kumaliza mapumziko yao Agosti 30

Muktasari:

Wachezaji wa timu hiyo walipewa mapumziko ya wiki moja baada ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini, ambao Serengeti Boys ilishinda kwa mabao 2-0 na kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-1. Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti Boys na Kongo Brazaville utapigwa nchini Septemba 18 kabla ya kurudiana majuma mawili baadaye.

Dar es Salaam. Kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kitaingia kambini Agosti 30 kujiandaa na mchezo dhidi ya Congo Brazaville wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana.

Wachezaji wa timu hiyo walipewa mapumziko ya wiki moja baada ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini, ambao Serengeti Boys ilishinda kwa mabao 2-0 na kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-1. Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti Boys na Kongo Brazaville utapigwa nchini Septemba 18 kabla ya kurudiana majuma mawili baadaye.

Kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema wachezaji walipewa mapumziko baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu na baada ya kurejea kambini wataendea na programu ya maandalizi kabla ya kucheza na Congo.