Simba Vs Yanga: Mashabiki wavunja geti, Nape atetea mfumo

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye

Muktasari:

Mashabiki wamevunja mageti la upande kushoto kutokea chuo cha Duce na kuingia ndani jambo linalowalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Mashabiki waliofurika katika mageti wameshindwa kuingia uwanjani kutokana na mashine kushindwa kufanya kazi vizuri na kusababisha wavunje mageti mawili.

Mashabiki wamevunja mageti la upande kushoto kutokea chuo cha Duce na kuingia ndani jambo linalowalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Mashabiki hawaelewi wanadai wamepanga foleni kwa muda mrefu, lakini hakuna kinachoendelea. Wengine wanataka kuingia uwanjani kwa kuonyesha kadi tu za selcom, lakini wanakataliwa.

Uwanja ndani bado ni mweupe hakuna mashabiki na wengi wapo nje wakishindwa kuingia.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema ni mapema kusema mfumo umeshindwa kazi tunapaswa kusubili baada ya mechi ndiyo tuseme.

“Kwanini mnapenda kuzungumzia mabaya tu, tupeni muda mwisho wa mchezo tutajua kama mfumo umeshindwa au la, lakini sasa ni mapema kusema hivyo,” amesema Nape kifupi.