Simba bado yamtaka Okwi

Mshambuliaji  wa Simba wa  zamani Emmanuel Okwi

Muktasari:

  • Okwi kipenzi cha mashabiki wa Simba kwa sasa yupo Uganda akiichezea Villa baada ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Denmark.

Unguja. Uongozi wa Simba bado unafuatilia nyendo za mshambuliaji wake wa zamani Emmanuel Okwi mambo yakienda vizuri watamrudisha kikosini.

Okwi kipenzi cha mashabiki wa Simba kwa sasa yupo Uganda akiichezea Villa baada ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Denmark.

Rais wa Evance Aveva alisema:"Kwa sasa ni mapema kuzungumzia suala la Okwi ukifika wakati mtajua hatuwezi kuwaaminisha watu kuwa anakuja halafu mwisho wa siku ikawa kimya."

"Ni kweli tunamfuatilia huko aliko anavyocheza ili kufahamu kiwango chake,"alisema Aveva.