TFF yatupa jicho Kundi B

Muktasari:

Kundi B lina timu za Njombe Mji, KMC, Polisi Moro, Mbeya Warrious, Coastal Union, JKT Mlale na Kurugenzi baada ya Kimondo kujitoa.

Dar es salaam. Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imetoa onyo kwa timu za ligi daraja la kwanza hasa zilizopo Kundi B, kutojihusisha na aina yoyote ya upangaji matokeo katika mechi za mwisho za ligi hiyo mwishoni mwa wiki hii.
Kundi B lina timu za Njombe Mji, KMC, Polisi Moro, Mbeya Warrious, Coastal Union, JKT Mlale na Kurugenzi baada ya Kimondo kujitoa.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema tunafahamu kuwa kwenye Kundi B kuna timu tatu ambazo kila moja ina nafasi ya kupanda Ligi Kuu kutegemeana na matokeo ya mechi zao za mwisho.
Shirikisho limechukua hatua madhubuti kuhakikisha hakuna upangaji wa matokeo kwenye mechi hizo kwani.
"Tumepeleka maofisa wetu kufuatilia kwa ukaribu kila tukio yote ya mechi hizo, pia tumezitaarifu mamlaka zote za ulinzi na usalama, kushirikiana nasi katika kudhibiti vitendo vya rushwa na upangaji wa matokeo," anasema Lucas.