Simba yaifunika Yanga nje ya uwanja

Muktasari:

Katika matawi mbalimbali mashabiki wa Simba wameoenekana kuchangamka zaidi kuliko watani zao Yanga na hivyo kuonyesha kuwa Wekundu wa Msimbazi wanajiamini zaidi katika mchezo wa leo.

Dar es Salaam. Simba imeonekana kujiamini kuliko Yanga wakati timu hizo zikielekea kupambana jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Gazeti hili limeshuhudia sehemu mbalimbali mashabiki wa Simba wakicheza na kufurahi kuliko Yanga.

Katika matawi mbalimbali mashabiki wa Simba wameoenekana kuchangamka zaidi kuliko watani zao Yanga na hivyo kuonyesha kuwa Wekundu wa Msimbazi wanajiamini zaidi katika mchezo wa leo.

Shabiki wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina la Ally Shabani anasema anawaangalia tu Simba jinsi wanavyofanya amsha amsha lakini jioni wasije wakazimia wote kutokana na kipigo watakachowapa.

Shabiki wa Simba, Mohammed Ally alijitapa kuwa wako vizuri dhidi ya Yanga hivyo watawapiga nyingi na ndio maana mashabiki wao hawana furaha kwa sababu wanajua kitakachowakuta jioni.